Mafinikio ya Kampeni ya OKOA

2016

Aprili

Kampeni iliyodumu kwa muda wa mwezi mzima kupitia vyombo vya habari kwa ajili ya kuteketeza ghala la meno ya tembo la Tanzania pamoja na kutumia mtandao wa kijamii wa facebook kuhabarisha siku zilizosalia kuteketezwa kwa ghala la meno ya tembo la nchini Kenya mnamo tarehe 30 Aprili.

Machapisho ya kila siku katika mitandao ya kijamii, Twitter na Facebook pamoja na kampeni ya picha kupitia Facebook kuwaelezea sababu za  kuteketeza hadharani ghala la meno ya tembo la Tanzania.

Uchapishaji wa barua ya pili ya wazi kwa rais wa Tanzania, Dr. John P Magufuli, kwa ajili ya kuomba utekelezaji wa haraka wa kuteketeza hadharani ghala la meno ya tembo la Tanzania. Barua ilichapishwa katika gazeti la Mwananchi na mtandao, pia iliambatana na mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo, Dar es salaam. Hii ilipelekea kuchapishwa katika gazeti la Mwananchi na Tanzania leo, Katika mtandao wa kijamii wa jamii forum, katika blogu ya Issa Michuzi na Dar post.

Machi

Mahojiano katika vituo vitano vya redio (Redio Sibuka, Clouds FM, Redio One, Radio Free Africa na East African Radio) na vituo viwili vya Televisheni (Mlimani TV na ITV).

Tumeendelea kushirikiana na kikundi maarufu cha uchekeshaji cha Orijino Comedy katika kituo cha televisheni cha TBC1 ili kuendelea kuelimisha na kujenga uelewa juu ya malengo matatu ya kampeni ya OKOA.

Februari

Mahojiano katika vituo viwili vya redio, (Boma Hai FM, Clouds FM) na katika vituo viwili vya televisheni (Super Sport, Clouds TV).

Tulialikwa kuzungumza katika maonesho ya Kilimanjaro Marathon, Moshi ili kuelimisha juu ya janga la ujangili wa tembo na kutoa hoja juu ya uteketezaji wa ghala la meno ya tembo la Tanzania.

Kutoa mada juu ya janga la ujangili wa tembo katika shule ya kimataifa ya Moshi.

Kutumia elimu-burudani kuelimisha watanzania kuhusiana na ujangili wa tembo katika kipindi maarufu cha burudani cha Orijino Comedi.

Kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuitaka serikali kuchukua hatua madhubuti katika janga la ujangili linaloendelea baada ya tukio kubwa la ujangili lililo fanyika katika pori la akiba la Maswa. Taarifa ilihitaji kuanzishwa kwa operesheni dhidi ya ujangili na kuwakamata na kuwashitaki wafanya biashara wa meno ya tembo ambao kesi zao hazijashughurikiwa.

Januari

Kuchapishwa kwa makala mbalimbali zihusianazo na malengo ya kampeni katika gazeti la mwananchi, gazeti la Kiswahili linaloongoza Tanzania

Kampeni ya Okoa ilishiriki katika makala maaulum (special documentary) na kutoa ujumbe kuhusu janga la ujangili wa tembo katika Afrika ya mashariki na Africa ya kusini. Makala hii ilirushwa katika televisheni ya Taifa ya Kenya, NTV na televisheni ya Afrika ya Kusini, SABC TV.

2015

Desemba

Kutangazwa kimataifa kupitia mahojiano juu ya kampeni ya OKOA na gazeti la kimataifa la National Geographic, ambayo pia ilichapwa katika katika magazeti mawili ya kitanzania (The Citizen na The Guardian)

Makala maalum ilitolewa mwezi Desemba 2015 katika jarida la Fema ambapo nakala 30,000 zilisambazwa katika shule 600 nchini.

Uzinduzi wa wimbo wa kampeni ya OKOA Tembo wa Tanzania, tazama hapa!

Novemba

Kuchapishwa kwa barua ya wazi kwa Rais Magufuli katika gazeti la mwananchi na katiuka mtandao. Barua hiyo ilisainiwa na watanzania zaidi ya 30 wakiwemo wahifadhi, waandishi wa habari, na wafanya biashara. Barua ilizinduliwa katika mkutano wa kitaifa na waandishi wa habari na hii ilipelekea kutangazwa katika vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa. Nakala za barua zilifikishwa  kwa wabunge wote waliochaguliwa. Pia barua ilichapishwa katika magazeri ya Mwananchi, Tanzania leo, Africa geographic, Blogu ya michuzi, Dar post na Biz News. Sambamba na hilo tulifanya mahojiano katika vituo vya televisheni vya Azam, ITV, Star TV, Channel Ten, Sibuka TV, TBC na Agape TV.

Oktoba

Semina na warsha fupi katika maonyesho ya kusisitiza amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi yaliyoandaliwa na Fema katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Shinyanga.

Uundaji wa vikundi vya OKOA Tembo wa Tanzania katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi (Arusha, Iringa, Mbeya, Shinyanga).

Septemba

Mahojiano katika kituo cha televisheni cha Clouds TV na katika redio za jamii za morogoro (Redio Ulanga na Pambazuko FM)

Agosti

Kuzinduliwa kwa kampeni ya OKOA katika vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na redio tatu za kitaifa na mikoa. Tukio hili lilifanyika katika maadhimisho ya siku ya Tembo ulimwenguni (Agosti 12).

Kuanzishwa kwa tovuti ya kampeni, Facebook na Twitter.

Warsha fupi na hotuba katika maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika Arusha, ambapo zaidi ya watu 500 walisaini kuunga mkono kampeni.