Maelezo Zaidi Kuhusu Malengo ya Kampeni

Kampeni hii ina dhumuni la kuunganisha sauti za Watanzania wote dhidi ya janga la ujangili wa Tembo na kushawishi  utekelezaji wa kukomesha janga hili. Kampeni hii ina dhumuni la kupata dhamira ya dhati kwa serikali ijayo kuchukua hatua tatu zifuatazo:

1.       Kuwakamata na kuwashitaki wafanyabiashara wakubwa wa meno ya tembo hapa nchini.

 Kwa kuwashitaki wafanyabiashara wakubwa wa meno ya Tembo kunaondoa motisha, vyanzo, na mianya yote ya ujangili wa Tembo kwa wafanyabiashara wa ndani. Kuwashitaki wafanyabiashara wakubwa wa meno ya Tembo kutavunja mitandao ya ujangili na kuwaondoa wengine kwenye kujihusisha na Ujangili na biashara haramu ya meno ya Tembo.

2.       Kutumia urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na China kufunga masoko ya meno ya Tembo huko China.

Takribani asilimia tisini (90%) ya meno ya Tembo toka Tanzania yanauzwa China ambapo biashara halali ya meno ya Tembo inatumika kama mwavuli wa biashara haramu ya meno ya Tembo ambacho ndio chanzo kikuu cha tatizo hili la ujangili wa Tembo. Tunaishawishi Serikali ya Tanzania kuiomba China kufunga masoko yote ya meno ya Tembo milele ili kuweza kulinda usalama wa muda mrefu wa Tembo hapa nchini. Kama mtumiaji mkubwa ya meno ya Tembo, kufunga biashara China kungepelekea kuanguka kwa haraka kwa biashara ya meno ya Tembo kwa sehemu nyingine ulimwenguni.

3.       Kuteketeza hadharani ghala ya meno ya Tembo Tanzania - kubwa kuliko yote ulimwengu.

Kutokana na kufungwa na mkataba wa kimataifa wa biashara juu ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka (Convention on International Trade in Endangered Species - CITES), Tanzania kwa sasa haiwezi kuuza ghala yake ya meno ya Tembo. Mwaka 2014 Tanzania ilisaini mpango wa kuwalinda tembo (Elephant Protection Inititative) uliozuia uuzaji wa meno ya Tembo kwa muda wa miaka kumi. Hata hivyo, uwepo wa ghala hii ya meno ya Tembo inawapa moyo wafanyabiashara haramu wa meno ya Tembo kuwa biashara itaendelea tena. Uuzaji wa ghala ya meno ya Tembo hauendani na usitishaji wa biashara ya meno ya Tembo, na mauzo yaliyopita ya maghala ya meno ya Tembo yalihamasisha biashara haramu ya meno ya Tembo. Kuharibu ghala ya meno ya Tembo kunatuma ujumbe mzito kwa majangili wa Tembo, wafanyabiashara wa meno ya Tembo na watumiaji kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa na kuwa ujangili wa Tembo ni kosa la jinai lisilokubalika.

Ni gharama kuitunza na kulinda ghala ya meno ya Tembo Tanzania – kuendelea kutunza meno ya Tembo ghalani ni kupunguza bajeti ya Taifa.

Nchi nyingi za Afrika zimeonesha dhamira zao kwa kuteketeza ghala za meno ya Tembo. Walipongezwa sana kimataifa kwa kufanya hivyo, na uteketezaji wa ghala za meno ya Tembo uliongeza ufadhili wa wahisani kwa uhifadhi na kupambana na ujangili.

Fedha nyingine nyingi zinaweza kupatikana kupitia utalii wa wanyamapori - chanzo cha mapato ambacho kinakua kinajitosheleza na kina manufaa kwa Watanzania wengi kwa muda mrefu – kuliko kuuza mara moja tu kwa ghala ya meno ya Tembo ambako kunaweza kuwezesha ujangili zaidi na kupelekea upotevu wa Tembo wa Tanzania.