Tembo wanauawa sana Tanzania.

Mwaka 1970, kulikuwa na Tembo 300,000 nchini Tanzania. Kulikuwa na Tembo 109,000 mwaka 2009, na Tembo 43,330 tu mwaka 2014.

 
 

Sababu hii yote ya ujangili ni mahitaji ya meno ya Tembo – kwa ajili ya kutengenezea sanamu na mapambo mengine. Hadi 90% ya meno ya Tembo wa Tanzania zinakwenda China, ambapo kisheria kuna soko la ndani la meno ya Tembo. Soko hilo halali linasaidia ufanisi wa soko haramu la meno ya Tembo. Njia pekee ya kuweka usalama kwa Tembo ni kupiga marufuku biashara yote ya meno ya Tembo milele, na kuharibu meno yote ya Tembo yaliyobaki kwenye maghala.

Tembo ni urithi wetu, na ishara ya taswira nzuri kwa Tanzania. Watu huja kutoka duniani kote ili kuona Tembo na wanyamapori wengine, na utalii huu unajumuisha 17% ya Pato la Taifa, na inasaidia 1,200,000 ajira ya Watanzania.

Hebu tuokoe Tembo wa Tanzania kabla ya kuchelewa mno. Kama ungependa kuona uharibifu wa urithi huu wa Tanzania unakomeshwa, tafadhali jisajili kwa ahadi OKOA TEMBO WA TANZANIA, ili kuonyesha msaada wako wa malengo haya matatu ya kampeni hii.

 

MALENGO YA ‘OKOA TEMBO WA TANZANIA’

1.  Kuhamasisha utekelezaji wa Sheria dhidi ya wafanyabiashara wakubwa wa       meno ya Tembo Tanzania.

2.  Kuisisitiza Serikali ya Tanzania kuweka msukumo kwa nchi ya China kufunga        soko la meno ya Tembo.

3.  Kuishawishi Serikali kuteketeza ghala ya meno ya Tembo Tanzania.

Kwa maelezo zaidi kuhusu malengo ya kampeni, bofya hapa

 
 

Jisajili kwa ahadi

Jina *
Jina